Leseni za zamani mwisho Machi 31
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mohammed Mpinga
amewataka madereva wote nchini kubadilisha leseni zao za zamani kwa kuwa
zimebaki siku saba tu zoezi hilo kumalizika, vinginevyo hatua za
kisheria zitachukuliwa.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mpinga alisema Machi 31, mwaka huu itakuwa mwisho wa madereva wote kutumia leseni za zamani, na kwamba kwa waliokuwa bado hawajabadilisha wafanye hima kubadilisha ili kuepuka usumbufu utakaojitokeza.
“Machi 31 ndiyo mwisho na hatutaongeza muda wa kubadilisha leseni, hivyo wananchi wakae wakijua, nawaomba watumie wiki hii moja iliyobaki kubadilisha leseni zao,” alisema Mpinga.

Post a Comment