ad

ad

JE WAJUA MADHARA YA MITANDAO YA KIJAMII?



Leo nimerudi na mada nyingine ya mahusiano, na katika mada yetu ya  leo sio ndefu ila ina swali mengi yasiyo na majibu.kwamba “je unajua kuwa  mitandao ya kijamii inaongoza kwa uvunjani wa mahusiano ya kimapenzi?”
 
Mitandaoya kijamii inatajwa kuwa ndio inayoongoza kwa kuvunja ndoa na mahusiano yasiyo rasmi ya kimapenzi,

Uchunguzi uliofanywa na watafiti unaonyeshwa mitandao hiyo huvunja mahusiano hayo kutokana na Ama MKE AU MUME, Girlfriend au Boyfriend  kuitumia mitandao hiyo kwa kuweka picha zao za nusu utupu, je? Ni nani unataka aone maungo hayo? Au ni sehemu ya kujitangaza kibiashara binafsi? 

Kati ya picha hizo mbaya zaidi ni za wadada,ambazo maungo yake yanamshawishi mwanaume kumtumia Friend Request.  Utafiti unaonyesha kuwa mtu anaetumia mitandao hiyo yaani Facebook, Twiter, Waasap, na kadhalika huwa wakali wapenzi wao wanapotaka kusoma sms zake hasa za inbox unakuwa ugomvi mkubwa. Jiulize je picha unazoziweka  zina mtazamo mzuri kwa jamii?
 
Moja ya wanaotajwa kutia fora kuweka picha hizo au kuvaa nguo za utupu na kupiga picha kisha kuziweka kwenye mitandao hiyo wakiwemo  waigizaji wetu wa filamu na muziki wa kizazi kipya.

Je ni kweli kwamba hatujui kuwa nguo tunazovaa ni nusu uchi au ni maonyesho ya nguo zenu za ndani ili tuzione?  Familia zenu zinaichukuliaje hali hiyo, Wanajamii wanawapenda kwa mavazi hayo au inawatazama kwa jicho la kingono?   

NINI MAANA YA MAADILI? HIVI HAKUNA SHERIA INAYOZUIA MTU KUONYESHA NUSU YA SEHEMU NYETI?
BADILIKENI:
Powered by Blogger.