HIVI NI KWELI WANAWAKE WAZURI SANA HAWAOLEWI ?
Uchunguzi
wa kina unaonyesha kwamba wanawake
wengi waliojaaliwa na mwenyezi
Mungu Uzuri saana wa maumbo yao na sura zao hawaolewi,
Uchunguzi huo uliofanywa na mwandishi wetu wa www.2jiachie.com
unaonyesha wanawake watu wazima, au wasichana wanaochipukia ikiwa wamejaaliwa
uzuri ule wa asili,na sio ule wa kununua, kama weupe wao,au maumbo yao
yaliyojaa vizuri kila idara ya viungo vya miili yao,
Ngumu
sana kuona wameolewa, uchunguzi huo ulioambatana na maswali kadhaa kutoka kwa
akina dada wenyewe na baadhi ya wanaume umejaribu kumfanya mwandishi wetu kujiuliza maswali mengi bila kupata majibu sahihi.
Mwandishi wetu ametimba mpaka
maeneo ambayo wanaume wengi hujiuliza
maswali wanapowaona wadada hao katika mishe mishe zao za style ya kutafuta
maisha.
1. Sehemu za starehe yaani clubs
2. Baa kubwa kubwa nchini.
3. Maeneo wanayopatikana madada
poa
Madada wa kwenye baa wengi majibu yao yalikua kama ifuatavyo.
Mwandishi:
Dada wewe mzuri sana, unaefaa
kuwa mke wa mtu, unafikiri ni kwa nini unafanya kazi hii
ambayo haina heshima kwa wanaokuona wanakuona kama malaya ?
Mhudumu wa baa:
Aaa kaka wanaume wengi ni
michosho tuu, ukitoka kidogo akirudi maswali meengi kama polisi, mi
nilishaolewa na nikaona michosho ya kupelekana
puta nikaamua kuachana na mume wangu na kuangalia mambo yangu, si unaona
hii pete kaka, ni ya ndoa kabisaa ya kanisani.
Na hayo ndio majibu ya karibuni
wadada woote aliopata nafasi ya kuwauliza maswali sehemu zoote silizooanishwa
hapo juu.
Na wengine wa madada hao ni wasanii
maarufu hapa Tanzania wa Bongo movie na wa musiki wa kizazi kipya. ‘Bongo
fleva’ na baadhi ya watoto wa vigogo serikalini,na wenye nafasi kubwa ya
kifedha nchini.
Majibu ya wanaume wengi
walijibu kama ifuatavyo:
“Wanawake wazuri sana ni
ugonjwa wa moyo,” “Wanaringa kuolewa kutegemea uzuri wao,” “Mwanamke mzuri
lazima uwe na hela, Ili wenye hela wasikuzidi maarifa kwa hela zao”
Mmoja wa wanaume hao walipiga
saluti kwa wadada mungu alivyowapendelea maumbo na kusema:
“Aaaa brother mi naogopa hata
kuwaanza, na wanawake wengi hawana mapenzi ya dhati kwa dunia ya sasa,
wanachoangalia wasilahi yao binafsi na sio ya kifamilia.
Jamani wapenzi wa ukurasa huu
wa mahusiano,Nisaidieni kuongeza majibu ya walionijibu
Majibu niliyopewa ni sahihi kwa
ufahamu wako?
Unafikiri ni kwa nini warembo
hao hawaolewi?
Kazi kwenu.
Habari na king love www.2jiacjie.com

Post a Comment