ad

ad

YAYA TOURE ARUDI NA MKWARA KWA MANCHESTER UNITED

MANCHESTER, ENGLAND
KIUNGO wa kimataifa wa Ivory Coast, Yaya Toure, amesema kuwa amerudi kuizuia Manchester United kutwaa ubingwa wa Premier League.
Toure jana usiku amewaonya wapinzani wao wakubwa, United akisema “mbio za ubingwa bado sana kufika mwisho.”
Staa huyo wa Manchester City amerejea kutoka Kombe la Mataifa ya Afrika akiapa kuisaidia timu yake kufuta pengo la pointi tisa kati yao na vinara United.
City ilitoka nyuma pointi nane msimu uliopita na kutwaa ubingwa mbele ya United, na sasa staa huyo anaitumia kumbukumbu hiyo akisisitiza: “Nina hakika tutarudi.
"United ina kikosi madhubuti na kweny egazeti wana safari nyepesi kuliko sisi, lakini mbio za ubingwa ni safari ndefu kufika mwisho.”
Alisema kuwa matokeo mazuri ndiyo yatawarudisha kwenye mstari, na kwamba sasa wanarudi katika hilo.
Powered by Blogger.