LUIZER MBUTU KUZALIWA UPYA JUMAMOSI MANGO GARDEN
BENDI ya African Stars “Twanga Pepeta” imemwandalia kiongozi wa bendi hiyo, Luizer Mbutu sherehe kubwa ya
siku yake ya kuzaliwa (Birthday Party) itakayofanyika Jumamosi tarehe
09-02-2013 katika ukumbi wa Mango Garden uliopo Kinondoni jijini Dar es
salaam.
Luizer
Mbutu hii ni mara ya pili kufanyiwa sherehe hiyo ambapo kwa mara ya
kwanza ilikuwa ni mwaka jana ndani ya Club ya Maisha, Oysterbay jijini
Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa mmoja wa wasenaji wa Twanga Pepeta, Hassan Rehani ASET
imeamua kumfanyia Luizer Mbutu sherehe hiyo kwa mara ya pili mfululizo
kwa kutambua mchango wake mkubwa alioutoa katika bendi ya Twanga Pepeta
kwa kudumu kwa muda mrefu bila kuhama na kwa kufanya kazi kwa kujituma
bila ya kuchoka.
Sambamba
na sherehe hiyo, Rehani amesema Twanga Pepeta kama ilivyo kawaida yao
watainogesha sherehe hiyo ya Kiongozi wao kwa masebene matamu
yatayoendana na nyimbo nzuri zilizo na meseji zilizojitosheleza kutoka
kwa wanamuziki wenye vipaji vya viwango vya hali ya juu.
Hassan
Rehani ameongeza kuwa wadau mbalimbali wamealikwa kuhudhuria sherehe
hiyo ili kutoa sapoti kwa Kiongozi huyo wa Bendi katika siku yake ya
kuzaliwa kwa kuwa utatumika utaratibu kama wa mwaka jana wa kulishwa
keki kwa wadau na marafiki walio karibu na bendi ya Twanga Pepeta.

Post a Comment