HARUSI YA 2FACE KUFANYIKIA DUBAI
LAGOS, NIGERIA
ACHANA
na wenye fedha! 2Face Idibia na mwenza wake Annie Macaulay wametangaza
kwenda kufanya harusi yao Dubai badala ya Abuja kama ilivyotangazwa
awali.
Annie ameanika hayo kwenye ukurasa wake wa Facebook, huku akitaja siku ya harusi yao kuwa Machi 23, mwaka huu.
2Face ambaye ni msanii wa muziki na Annie wa filamu, tayari wamefunga ndoa ya kimila Mei 2, mwaka huu, ambayo ilikuwa ya siri.
Annie
alikwenda Dubai hivi karibuni kununua vifaa kwaajili ya ndoa na kufanya
‘booking’ ya ukumbi kwaajili ya sherehe ya harusi yao.
Pia alikwenda New York, Marekani kununua gauni lake la harusi.
Habari
zimepasha kuwa, wawili hao wamepanga kwenda Dubai pamoja na marafiki
wachache na ndugu wafamilia, ambao watakodiwa ndege maalumu.
Kwamba
tayari wawili hao wamefanya ‘booking’ ya vyumba kadhaa kwenye hoteli
chache huko Dubai, ikiwemo Burj Al Arab – hoteli ya kifahari zaidi
duniani, ambayo wenza hao pia watakwenda ‘kujiachia’ baada ya ndoa yao.

Post a Comment