ad

ad

FM ACADEMIA KUTAMBULISHA NYIMBO MPYA KAWE IJUMAA HII

BENDI ya FM Academia “Wazee wa Ngwasuma “ Ijumaa hii watatambulisha nyimbo zao mpya katika ukumbi wa Masae Garden View uliopo Kawe.
Akiongea na Saluti5, msemaji wa kundi hilo, Kelvin Mkinga amesema katika onyesho hilo bendi yake itatambulisha ‘silaha’ zao zote zitakazokuwemo katika albam yao mpya itakayojulikana kama “Chuki ya nini” ambayo itazinduliwa baadae mwaka huu.
Aidha, Kelvin amesema mbali na nyimbo mpya, pia watashusha rap zao mpya ikiwemo ile ya Ugali kwa kachumbari.
Powered by Blogger.