Endless Fame Film Ofisi babukubwa ya Wema Sepetu hii hapa
SI OFISI ya kitoto, ni ofisi ya bab kubwa iliyokwenda shule ikiwa imepambwa kwa fanicha na mashine za kisasa.
Naam
hiyo ndio ofisi ya Wema Sepetu, mlimbwende na muigizaji nyota wa
filamu, ni ofisi itakayobeba kazi zake za kila siku kupitia kampuni yake
ya Endless Fame Film.
Akizungumza
na waandishi wa wa habari masaa kadhaa yaliyopita wakati akiitambulisha
rasmi kampuni yake, Wema Sepetu alisema Endless Fame Film
itajishughulisha na utengenezaji wa filamu pamoja na kuandaa matamasha
mbali mbali.
Ofisi za Wema Sepetu zitakazoanza kazi rasmi mwezi ujao zipo Mwananyamala koma koma, Dar es Salaam.

Sehemu ya kumpuzika wageni


Mandhari ya ofisi kwa juu

Wema akiwa na Mama yake


Sehemu nyingine ya ofisi inavyoonekana

Post a Comment