ad

ad

CASSIM MGANGA KUPELEKA UTAJIRI WA MAHABA LINDI NA MTWARA



MWIMBAJI mkali wa nyimbo za mahaba Cassim Mganga wiki anatarajiwa kufanya maonyesho matatu katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
Maonyesho hayo yamechukuliwa kama mwendelezo wa shangwe za msimu wa wapendanao ambapo Ijumaa hii Cassim atakuwa ndani ya ukumbi wa BR uliopo Masasi mkoani Mtwara.
Jumamosi Cassim atakuwa Lindi mjini katika ukumbi wa Paris Club kabla ya Jumapili kuelekea Mtwara mjini na kufanya onyesho lake la mwisho kwenye ukumbi wa Maisha Club.
Miongoni mwa nyimbo zinazomfanya Cassim asubiriwe kwa hamu kubwa na wakazi wa mikoa hiyo ni “Tajiri wa Mahaba”.
Powered by Blogger.