ad

ad

THEO WALCOTT AKUBALI KUBAKI ARSENAL


 HATIMAYE Theo Walcott amekubali mkataba mpya Arsenal na nyota huyo wa timu ya taifa England mwenye umri wa miaka 23, leo anatarajiwa kusaini mkataba wa pauni 100, 000 kwa wiki, linaandika la gazeti la The Sun.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amethibitha: “Natumai mkataba utakuwa umesainiwa kabla ya wikiendi. Kuna uwekezakano. Kwa mtazamo wangu ni asilimia 99 sasa.
Wenger alikuwa anahofia kumpoteza mshambuliaji huyo baada ya mvutano juu ya mkataba wake na alihofia kuwa amepoteza mchezaji mwingine mkubwa.
Kocha huyo ameshuhudia majina makubwa kama Cesc Fabregas, Samir Nasri, Robin van Persie na Alex Song wakiondoka klabuni ndani ya misimu miwili.
Wenger alikiri: “Kutokana na uzoefu nilioupata, niliingia woga katika hatua fulani kwamba angeweza kuondoka .
“Wakati mambo yanapochukua muda mrefu, si dalili nzuri.
“Imetuchukua muda mrefu kufika tulipotaka. Bado halijakamilika, lakini tunatumai hadi wikiendi litakuwa limekwisha”
Powered by Blogger.