Alex Ferguson amesisitiza kuwa timu yake siyo tegemezi kwa Robin Van Persie.
Robin
Van Persie ameanza kwa kishindo maisha mapya ndani ya Old Trafford
akifunga magoli 21 yakiwemo 10 aliyofunga katika mechi 10 zilizopita.
Lakini Fergie anakataa kuwa United haibebwi na Van Persie. “Sikubaliani na fikra hizo kuwa tumekuwa timu ya mtu mmoja.
“Katika
historia yetu kuna wakati tulibebwa na mtu mmoja. Eric Cantona
alituweka mashindanoni kwa magoli yake huku wenzake wakiwa wamechemsha.
“Lakini vitu ni tofauti kwa sasa.
“Javier Hernandez tayari ana magoli 12 huku Rooney akiwa na mabao 9.
“Mabeki wawili, John Evans na Patrice Evra kwa pamoja wana magoli 8, kwahiyo hamaanishi kuwa ni timu ya mtu mmoja.
Kocha
wa Manchester City, Roberto Mancini alisema mapema mwezi huu kuwa
kushindwa kwao kumsajili Van Persie kunaweza kuwagharimu kulitema taji
lao.
Ferguson
anakubaliana na mpinzani wake kuwa mshambuliaji huyo wa pauni milioni
22 anaweza kuleta tofauti ifikapo mwezi Mei (Mwisho wa msimu).
Aliongeza: ‘Hakika anafurahia changamoto yake mpya, ni mchezaji sahihi, katika timu sahihi, katika wakati sahihi.

Post a Comment