BAYERN MUNICH YAIBUKA MBAMBE VITA VYA KUMSAKA GUARDIOLA
MUNICH, UJERUMANI
BAYERN
MUNICH imeshinda vita ya kuwania kumsainisha Pep Guardiola,
aliyeibebesha Barcelona mataji 14 ndani ya misimu minne aliyokuwapo Nou
Camp.
Taarifa hiyo imekuwa mwisho wa klabu kadhaa za Premier League, zikiwamo Manchester City na Chelsea zilizokuwa zikimfukuzia.
Kocha
huyo Mhispania mwenye miaka 41 pia alikuwa akihusishwa na klabu za
Arsenal na Manchester United — endapo Arsene Wenger na Alex Ferguson
wangeachia ngazi.
Lakini
baada ya miezi kadhaa ya tetesi za hapa na pale, kocha huyo amechagua
kujiunga na miamba hiyo ya Ujerumani kuanzia mwezi Julai.
Guardiola,
ambaye anautumia msimu huu kwa mapumziko jijini New York, Marekani
amesaini dili la mkataba wa miaka mitatu Allianz Arena.
Mtendaji
Mkuu wa Bayern, Karl-Heinz Rummenigge alisema: “Tuna furaha kubwa
kwamba tumefanikiwa kumshawishi mtaalamu wa soka, Pep Guardiola, ambaye
alikuwa akihitajika na kuwasiliana na klabu nyingi kubwa, kuja Bayern
Munich.
“Guardiola
ni mmoja wa makocha wenye mafanikio makubwa duniani na tuna hakika
kwamba anaweza kuleta mafanikio makubwa si kwa Bayern Munich pekee,
lakini pia kwa soka ya Ujerumani kwa ujumla.”
Guardiola atachukua mikoba kutoka kwa Jupp Heynckes ambaye aliamua kutoongeza mkataba wake, na atastaafu.
Kabla
ya kumwaga wino Bayern, Guardiola alisema ana nia ya kwenda England
kufundisha soka katika moja ya klabu za Premier League siku za usoni.
Alisema hayo katika ujumbe wa video alioutuma kwa Chama cha Soka England (FA) kukipongeza kutimiza miaka 150 tangu kuanzishwa.
"Kama mchezaji, sikuweza kutambua ndoto yangu kucheza huko," alisema.
"Lakini
natumaini, katika siku zijazo, nina changamoto kuwa kocha huko na
kuhisi uzoefu wa makocha wote na wachezaji ambao wamekuwa huko.
"Ni
ya kipekee, kucheza katika ligi ile (Premier League). Nataka kuhisi
mashabiki, mazingira, vyombo vya habari na staili ya wachezaji. Mara
zote nimebaini soka ya Kiingereza inavutia. Sapoti kwa timu ya nyumbani
ni ya kushangaza.
"Ndani
ya Italia, Latini watu watakusapoti wakati mnapocheza, na endapo
utapoteza, watakuua. Ndani ya England, mara zote nimeshangazwa kwamba
watu wanasapoti kila kitu.
"Hiyo
ni nzuri na kwanini, labda, mimi bado ni kijana, kama miaka 41 tu,
natumaini kuwa na changamoto au fursa ya kutoa mafunzo huko."
Post a Comment