AMANDA POSHY AMCHARUKIA MWANAMKE MWENZAKE ALIYEMTONGOZA
MSANII
mwenye jina kubwa katika tasnia ya filamu, Amanda Poshy amemjia juu
mwanamke mwenzake aliyemtongoza kuhusu ngono ya jinsia moja.
Amanda
ameiambia Saluti5 jana jioni kuwa mwanamke huyo anayejiita Vicky Maya
alimtumia ujumbe kupitia facebook na kumuuliza kama wanaweza kushiriki
tendo la jinsia moja.
Amanda Poshy
“Simjui
huyo mwanamke, aliniomba urafiki kwenye facebook nikampokea, matokeo
yake ananiletea mambo ya kishenzi ya kusagana, nimempa vipande vyake
asifikiri kila mtu ni mshenzi” alisema kwa hasira Amanda.
Kama
vile hiyo haitoshi jana usiku Amanda akaamua kumuanika mwanamke huyo
kwenye ukurasa wake wa facebook kwa kuandika: “VICKY MAYA naomba
ujiheshimu....me nina mtu wng na najiheshimu tena ninaheshimika kwenye
jamii iliyonizunguka.....huo upuuzi wako unaoniandikia inbox kuhusu
kusagana me sisagani katafute wacyojiheshimu wenzio kama ww uwaambie
upuuzi kama huo.......tuheshimiane”.
Vicky Maya
Amanda
alisema mwanamke huyo kwenye wasifu wake amejitambulisha kama binti
aliyezaliwa 5 Machi 1988, mkazi wa Masaki Dar es Salaam.
Post a Comment