Yanga Yatwaa Ubingwa wa 32 Ligi Kuu Tanzania Bara Msimu 2025/26
Young Africans SC (Yanga SC) wametawazwa rasmi kuwa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2025/26, ikiwa ni ubingwa wao wa 32 katika historia ya klabu hiyo.
Yanga wametwaa taji hilo kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, wakifanikiwa kutetea ubingwa wao kwa mara ya tano mfululizo.
Mabao ya Yanga katika mchezo huo yalifungwa na Stephane Aziz Ki (Dube) dakika ya 8, Maxi Nzengeli dakika ya 51 na Clement Mzize (Depu) dakika ya 66.
Kwa matokeo hayo, Yanga SC wamemaliza msimu wakiwa na pointi 75, wakizidiwa kwa tofauti ya pointi mbili na wapinzani wao wa jadi Simba SC waliomaliza nafasi ya pili wakiwa na pointi 73 baada ya michezo 30.
Azam FC imemaliza nafasi ya tatu ikiwa na pointi 62, huku Singida Black Stars wakikamilisha top four kwa pointi 50.
Mfungaji Bora
Mshambuliaji wa Singida Black Stars, Mosi Ndumumwe, ameibuka mfungaji bora wa ligi msimu wa 2025/26 baada ya kufunga jumla ya mabao 17. Ndumumwe alihitimisha msimu kwa hat-trick katika mchezo uliomalizika kwa Singida BS kupoteza 4-3 dhidi ya Fountain Gate FC.
Matokeo Mengine
Simba SC 1-0 KMC FC – Loemba (penalti) 55’
Azam FC 2-0 Dodoma Jiji – Ngita 67’, Chilambo 90+’
Mashujaa FC 0-1 Tanzania Prisons – Lulihoshi 90’ (penalti)
Mbeya City 0-0 TRA United
Coastal Union 2-1 Pamba Jiji
Namungo FC 2-1 Mtibwa Sugar – Luzendaze 33’, Masawe 85’ / Evanc 01’
Fountain Gate 4-3 Singida BS – Mossi alifunga hat-trick katika mchezo huo wenye mabao mengi
Kwa ushindi huo, Yanga SC wanaendeleza rekodi yao ya ubabe katika soka la Tanzania Bara, huku ligi ya msimu huu ikimalizika kwa ushindani mkubwa kati yao na Simba SC.
.jpg)
Post a Comment