ad

ad

Yanga Watangaza Viingilio vya Mchezo wa CAFCL Dhidi ya JS Kabylie Zanzibar



 


Klabu ya Young Africans (Yanga SC) imetangaza rasmi viingilio vya mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) dhidi ya JS Kabylie, utakaochezwa Februari 15, 2026 katika dimba la New Amaan Complex, Zanzibar.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa huku Yanga wakihitaji matokeo mazuri ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele katika michuano hiyo ya kimataifa.

Mashabiki wa Wananchi wanatarajiwa kujitokeza kwa wingi kuipa sapoti timu yao, huku kauli mbiu yao ikiwa #TutafuzuKwaKishindo, wakiamini ushindi nyumbani utakuwa chachu ya mafanikio.

Uongozi wa klabu umehimiza mashabiki kununua tiketi mapema na kujaza uwanja ili kuipa timu morali katika pambano hilo muhimu.

No comments

Powered by Blogger.