Sanchi Azua Kicheko Mtandaoni kwa Kauli Yenye Mafumbo: “Ukikumbatia Sufuria la Moto”
Mrembo maarufu na modo anayeendelea kuteka mitandao ya kijamii nchini Tanzania, Jane Rimoy, almaarufu kama Sanchi (@surraiyaworld), ameendelea kuwa gumzo mitandaoni baada ya kuposti ujumbe wa mafumbo uliosababisha vicheko na mijadala miongoni mwa mashabiki wake.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Sanchi aliandika:
“Eti hivi mtu unajisikiaje ukikumbatia sufuria la moto? 😂😂 #KivutioChaTaifa 💋”
Kauli hiyo ya mafumbo ilichukuliwa na wengi kama mzaha uliobeba ujumbe wa ndani, huku baadhi ya mashabiki wakihusisha na hali za mahusiano au watu waliokwama katika mazingira magumu lakini bado wanayashikilia.
Post a Comment