ad

ad

MUDATHIR YAHYA ATOA KAULI KUHUSU HATMA YAKE YANGA SC

 


Kiungo wa kati wa klabu ya Yanga SC, Mudathir Yahya Abbas, ameweka wazi kuwa mkataba wake na mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara umeisha rasmi, huku akibainisha kuwa bado hajafanya uamuzi wa mwisho kuhusu mustakabali wake wa kisoka.

Akizungumza katika mahojiano maalum, Mudathir amesema kwa sasa yupo kwenye kipindi cha kutafakari huku akiwasubiri viongozi wa klabu hiyo kutoa mwelekeo wa nini kitafuata.

    "Mkataba wangu umeisha, hadi hivi sasa bado sijasaini. Nawasikilizia viongozi wangu. Wakinihitaji, nitaendelea. Mimi ni mfanyakazi," amesema kiungo huyo.

Mudathir, ambaye ni miongoni mwa wachezaji waliotoa mchango mkubwa kwa mafanikio ya Yanga katika misimu ya hivi karibuni, amekuwa sehemu ya kikosi kilichoshinda mataji kadhaa na kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika mwaka 2023.

Taarifa za kuhitimika kwa mkataba wake zimeibua minong’ono kuhusu mustakabali wake, huku baadhi ya klabu za ndani na nje ya nchi zikihusishwa kuwa na nia ya kumsajili.

Hata hivyo, Mudathir amesisitiza kuwa kipaumbele chake cha kwanza ni Yanga, akionyesha wazi kuwa hana haraka ya kufanya uamuzi hadi pale mazungumzo na uongozi wa klabu yatakapofikia tamati.

No comments

Powered by Blogger.