LAMEK LAWI AJIFUNGA MIAKA MIWILI KWA AZAM FC
MATAJIRI wa Dar, Azam FC hawataki utani kwa kuwa tayari wameanza kushusha mashine za kazi kuelekea msimu mpya wa 2025/26 kwa kumtambulisha beki wa kazi ambaye ni mzawa.
Julai 3 2025 mabosi wa Azam FC wamemtambulisha rasmi Lamek Lawi kwa kandarasi ya miaka miwili beki huyo ambaye alikuwa chaguo la kwanza ndani ya Coastal Union inayotumia Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Ni mchezaji wa kwanza kutambulishwa ndani ya Azam FC atakuwa mali ya timu hiyo iliyomaliza ligi ikiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo na pointi 63 baada ya mechi 30 mpaka 2027.
Coastal Union inaingia kwenye orodha ya timu tano ambazo zimefungwa mabao machache msimu wa 2024/25 licha ya kutokuwa kwenye mwendo mzuri.
Baada ya mechi 30 ukuta wa Coastal Union ni mabao 31 uliruhusu, nafasi 8 kwenye msimamo na pointi zao ni 35 kibindoni.
Post a Comment