Tunda Umbo Dogo Lakini ‘Kawapiga Pini, Dada Zake
SIKU
za nyuma kidogo, utakubaliana na mimi kwamba mastaa kama vile Wema
Sepetu, Irene Uwoya, Kajala Masanja, Jack Wolper na wengineo ndiyo
waliokuwa wakitawala kwenye vyombo vya habari kwa kila siku kuibuka na
vijimambo.
Kwa jina lingine tunaweza kusema, madada hawa walikuwa ‘scandal makers’ lakini sasa hivi wote kimyaaa, kabinti kadogo kenye umri usiozidi miaka 24 ambako kameonekana kwenye video za wanamuziki kadhaa Bongo ndiko kanakotamba kwa sasa.
MAISHA YAKE
Maisha yake yamekuwa yakiibua viulizo vingi sana kwani mara kwa mara amekuwa akionekana kwenye viwanja mbalimbali vya starehe bila watu kujua shughuli inayomuingizia kipato.
Maswali ni kwamba, anapata wapi hizo fedha za kujiachia kila siku? Mbona haonekani kufanya kazi ambayo imemtambulisha ya kuuza sura kwenye video ‘video queen’, kazi ambayo kimsingi hailipi kihivyo Bongo?
Watu wanahoji, hata kama anapewa na wazazi wake, haiingii mzazi aendelee kumruhusu mwanaye aponde raha kila siku bila kufanya jambo lolote la maana.
Kwa idadi ya kazi zake za video queen, kipato cha kazi yake hiyo ambayo inafahamika wengi wao hulipwa kidogo au kutolipwa kabisa, kamwe haiingii akilini kwamba ndizo zinazomuwezesha kufanya kufuru ya starehe kila uchwao.
Ukitembelea ukurasa wake wa Instagram, utaona jinsi ambavyo kila siku mrembo huyo yuko bize kwenye mahoteli makubwa akila na kunywa huku chanzo cha starehe hizo kikitajwa kuwa huenda ni vigogo wanamuwezesha.
Ukitazama pia aina ya picha anazopiga na kuweka kwenye ukurasa wake wa Instagram, zina viashiria fulani ambavyo si vizuri na watu kuhoji kwamba huenda akawa anafanya hivyo kutafuta soko la wanaume.
MSURURU WA WANAUME
Japo haiwezi kupatikana idadi kamili ya wanaume ambao ametajwa kuanguka nao dhambini lakini mrembo huyu anatajwa kama miongoni mwa warembo ambao wana msururu mrefu wa wanaume mastaa na wasio mastaa.
Kama hiyo haitoshi, Tunda pia anatajwa ‘kujiweka’ kwa watu wakubwa waliomzidi umri kama ilivyojidhihirisha hivi karibuni baada ya kuvuja kipande cha video kikimuonesha akifanya mambo ya kimalovee na mtoto wa marehemu Kingunge Ngombale Mwiru, Kinje.
Kwa mastaa wanaofahamika, Tunda alishawahi pia kudumu muda mfupi penzini na bwa’mdogo anayefanya muziki wa Hip Hop, Young D. Baadaye alimwagana naye, pia ameingia kwenye himaya ya staa wa Bongo Fleva, Diamond.
Usisahau ni Tunda huyuhuyu, iliwahi kuvuja video yake akiwa na mchekeshashi Stan Bakora wakifanya mambo ya chumbani.
NI KIVURUGE KWELI KWELI
Amemwagana na bwa’mdogo Young D ambaye kwa macho inaonekana kabisa ni saizi yake. Amehamishia majeshi kwa Diamond ambaye kidogo amemzidi yeye umri.
Diamond ana watoto wawili, amezaa na Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’. Amesababisha mpasuko mkubwa katika penzi hilo lakini pia, Tunda huyohuyo ametibua ndoa ya Kinje.
MATUKIO MABAYA
Tunda amekuwa akitajwa kuwa na mwenendo mbaya kutokana na maisha yake kutoeleweka nini hasa chanzo cha mapato yake. Aliwahi pia kutajwa kwenye orodha ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kujihusisha na madawa ya kulevya.
KAZI ZAKE
Ukiachana na ngoma za hivi karibuni, Tunda ni video queen ambaye ameonekana kwenye Wimbo wa Barnaba na Amini unaokwenda kwa jina la Why Me, wimbo wa Matonya aliomshirikisha Christian Bella wa Agwelina, wa TID unaoitwa Raha, wa Christian Bella, Dully Sykes na Tanzanite unaoitwa Ndombolo ya Solo na Wimbo wa Timbulo unaoitwa Sina Makosa ambazo ni za muda kidogo.
AJIFUNZE
Mambo anayoyafanya hayalingani na umri wake, ni vyema Tunda akajitambua. Akajua kwamba kuna maisha baada ya hizi starehe anazozifanya, kuna magonjwa na kuna matatizo makubwa yanayoweza kumpata kama tu ataendelea kuishi maisha ya anasa.
Namshauri atubu, atafute shughuli halali ya kufanya, akiendelea na mwenendo huu, mwisho wake utakuwa mbaya!

Post a Comment