Tottenham 2-0 Manchester United, Beki wa Man Utd Ajifunga
Meneja Mauricio Pochettino aliwasifu
sana vijana wake wa Tottenham kwa kuanza mechi kwa ukali baada ya
Christian Eriksen kufunga bao sekunde 11 pekee baada ya mechi kuanza, na
kufanikiwa kulaza Manchester United 2-0 uwanjani Wembley.
Ilikuwa siku ya miamba kulala kwani mabingwa watetezi Chelsea pia walilazwa 3-0 na Bournemouth, ushindi ambao meneja wao Eddie Howe ameueleza kuwa matokeo bora zaidi kwao Ligi ya Premia.
Mabao ya kipindi cha pili kutoka kwa Callum Wilson, Junior Stanislas na Nathan Ake yaliwahakikishia Bournemouth ushindi wao wa kwanza ugenini katika mechi saba za ligi, Chelsea nao wakaondoka uwanjani na kichapo kilichofikia kipigo kikubwa zaidi walichopokezwa msimu huu.
Bournemouth, ambao wanacheza ligi kuu msimu wa tatu pia walilaza Chelsea na Manchester United msimu wa 2015-16, Liverpool na Leicester msimu wa 2016-17 na Arsenal mapema mwezi huu.
Uwanjani Wembley, raia wa Denmark Ericksen alifikia mpira kutoka kwa Harry Kane na Dele Alli na kufunga bao ambalo kwa sasa ni miongoni mwa mabao ya tatu katika kufungwa kwa kasi zaidi Ligi ya Premia.
United walijibu vyema kujipata nyuma na karibu Jesse Lingard asawazishe lakini Phil Jones akaelekeza krosi ya Kieran Trippier na kujifunga dakika ya 28 na kuwaweka Spurs mabao mawili mbele.
"Unaweza kushinda mechi iwapo uko tayari kupambana. Ilitufaa sana kuanza vyema mechi," alisema Pochettino.
Meneja wa United Jose Mourinho alieleza bao hilo la kwanza kuwa "la kushangaza", na akaongeza kwamba: "Bao la pili kiakili huiua timu.
"Ili kushinda mechi timu inahitaji kufunga mabao na kujilinda vyema - wakati tulikuwa hafifu sana."
Kushindwa huko kulifikisha kikomo mkimbio wa United wa kutoshindwa mechi nane ligini na pia kupanua mwanya kati yao na viongozi Manchester United hadi alama 15.
Post a Comment