Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Al Haji Mussa Salimu Ampa ONYO Kali Mange Kimambi
Sheikh
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Al Haji Mussa Salimu amemjibu mwanadada
mkosoaji wa mtandaoni Mange Kimambi kwa kudai kuwa huu ndiyo mwaka wake
wa mwisho kutumia mikono pamoja na ulimi wake kutukana watu.
Sheikh
huyo amesema kwamba kutokana na kitendo hicho cha Mwanadada huyo
kumuanika mtandaoni na kumtolea maneno machafu yeye kama kiongozi wa
dini atarudi kwenda kushtaki katika mahakama ya mbinguni ambayo haina
rushwa.
Kauli
hiyo ya Sheikh Mkuu imekuja ikiwa ni siku moja tangu ianze kusambaa
picha yake mitandaoni na kuanza kutuhumiwa kuwa anashiriki katika
kampeni za uchaguzi mdogo kukisaidia Chama Cha Mapinduzi
"Tutarejea
katika mahakama ya mbinguni kwani mahakama ya Mwenyezi Mungu haina
rushwa na tutamuuliza Mwenyezi Mungu kama alimpa Huyu Mange Kimambi
mikono kwa ajilli ya kudhalilisha na kuvunja heshma za watu. Amekuwa
akiwatukana viongozi wa serikali lakini kwa hekima zao wamemnyamazia
kimya.
"Tunamuonya
acheze na namba nyingine lakini siyo viongozi wa dini kwani wao wana
mahakama ya kushatakia. Huu utakuwa mwaka wake wa mwisho kutumia ulimi
au mikono yake kudhalilisha watu".-Al Haji Mussa Salimu .
Hata
hivyo Sheikh huyo amesema kwamba wapo watu wengi waliompa rai ya
kutomjibu Mange Kimambi na kwamba kumjibu kwake kutamfanya atukanwe
sana lakini amesema kwamba mwanadada huyo aendelee kutukana kwani dua ya
mwenye kudhulumiwa haina kizuizi na kama anaishi hapa duniani basi
afahamu kwamba hataendelea kuwa salama na amejihalalishia mwenyewe kwa
ulimi wake na mikono yake.
Post a Comment