ad

ad

Sasha anadaiwa kulowea kwenye ulabu na kuwa chapombe

MWANADADA anayetikisa kwa umbo, Sasha Kassim anadaiwa kulowea kwenye ulabu na kuwa chapombe, kutokana na msongo wa mawazo siku chache baada ya uchumba wake na mwanaume wake wa Kizungu aitwaye Boniphace kuvunjika.

Mwanadada huyo amekuwa akionekana maeneo mbalimbali ya kula bata akifakamia pombe kali, jambo linaloonyesha wazi huenda ana ‘stress’ sababu alikuwa anatamani kuingia kwenye ndoa, lakini ndo’ hivyo tena imeota mbawa.

Sasha alipovutiwa waya juu ya ishu hiyo aliangua kicheko na kusema kuwa; “Watu bwana, kila anayekunywa pombe eti ana stress, ni kweli siku hizi nimekuwa cha pombe ndo starehe yangu ya sasa, ndiyo maana nimenenepa sana kwa sababu hiyo ya ulabu, ningekuwa nina mawazo ningekonda.”

No comments

Powered by Blogger.