ad

ad

Imevuja! Lulu Diva Apokonywa Kila Kitu na Mpenzi Wake!

 
Mwanamuziki wa kike anayekuja kwa kasi Bongo, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ akiwa pembeni ya gari mpya aina ya Jeep na nyumba aliyopewa na kigogo. 

IMEVUJA! Ukiachana na habari ya kudaiwa kupangishiwa nyumba na kununuliwa gari mpya aina ya Jeep na kigogo, imebainika kuwa msanii huyo amepokonywa kila kitu alichokuwa amepewa na mpenzi wake wa zamani aitwaye Joho.
Hivi karibuni, Lulu Diva aliripotiwa kuwa amepangiwa nyumba na kupewa gari jipya ambapo aliibuka sosi mwingine na kudai kuwa Lulu si mkweli, aliyenunua gari hilo ni mpenzi wake Joho ambaye alikuwa akiishi naye kinyumba kwa takriban miaka mitatu kiasi cha kufikia hatua ya kutolewa mahari ambayo ilirudishwa hivi karibuni na hata hivyo gari hilo amepokonywa hayuko nalo tena.
 

Lulu akiwa mbele ya gari aina ya Brevis.

Akipiga stori na Risasi Jumamosi kwa sharti la kutotajwa jina sosi huyo alisema kuwa anawajua vilivyo Lulu na Joho kwa sababu Joho ni rafiki yake hivyo anachokisema yeye ana uhakika nacho kwamba Lulu hajanunuliwa gari bali ni lile lile alilopewa na Joho.
“Hivi mnajua kuwa huyo Lulu ni muongo mbona gari analosema amepewa na kigogo ni la rafiki yangu Joho alimnunulia na walikuwa wakiishi pamoja ila kwa sasa ameachana naye na ninavyojua amechukua vitu vyake.
“Hii yote ilikuja baada ya jamaa kumshtukia kuwa Lulu anatembea na msanii mwenzake, Rich Mavoko,” alisema sosi huyo.

Baada ya habari hiyo kutua kwenye dawati la Risasi Jumamosi, Lulu alisakwa na kufunguka kuwa kweli alikuwa na mpenzi anaitwa Joho alimnunulia gali aina ya BMW na si hilo alilonalo kwa sasa kwani baada ya kugombana naye alimpokonya kila kitu chake ikiwemo na hilo gari.
“Yaani sitaki hata kukumbuka kwa kweli maana Joho alinitenda sana kiasi kwamba nilikuwa nikikesha nalia kwani alinifukuza hata kwenye nyumba aliyonipangishia na huwezi amini alinichukulia na gari hilo ambalo kwa mtu yeyote lazima alifananishe na hili kwa sababu ya rangi, hili la sasa ni Jeep jamani, lile lilikuwa ni BMW,” alisema Lulu.
 
Lulu Diva Akiwa na BMW
Hata hivyo, aliendelea kufunguka kuwa baada ya kuondoka kwenye nyumba ile aliyopangishiwa na Joho alihamia kwenye nyumba nyingine na kuwa na gari aina ya Brevis ambayo alijinunulia mwenyewe lakini baadaye aliiuza.
“Toka nimeachana na Joho nilimiliki gari aina ya Brevis lakini baadaye nalo nililiuza baada ya kumpata kigogo ambaye ameninunulia hili la sasa Jeep, kiukweli nina maisha mengine mazuri tu sitaki kukumbuka hayo yaliyopita,” alisema Lulu Diva.

Alipoulizwa kuhusiana na Rich Mavoko kuwa ndio aliyesababisha kuachana kwa yeye na Joho alisema kuwa Rich ni rafiki yake tu hayo mengine yeye hayajui.
“Jamani Rich ni rafiki yangu tu mimi hayo mengine siyajui,” alisema Lulu Diva.
STORI: Waandishi Wetu, Risasi Jumamosi

No comments

Powered by Blogger.