Chadema Hawamwamini Msimamizi Uchaguzi Kinondoni (Video)
CHAMA cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) leo wamesema hawana imani na msimamizi wa uchaguzi jimbola Kinondoni wakidai kuna
njama zilizopangwa dhidi ya chama hicho katika uchaguzi utakaofanyika wiki
ijayo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa
Mafunzo na Operesheni wa Chadema, Benson Kigaila , amesema baadhi ya njama hizo ni kuwepo
taarifa kwamba kuna watu walioletwa kutoka Zanzibar kuja kushiriki uchaguzi huo
wa Kinondoni ambapo amesema wapo kwenye hoteli na nyumba za kulala wageni eneo
la Kijitonyama, Kinondoni, jijini Dar es
Salaam.
Kigaila aliongeza kusemakwamba chama chake kimeona dalili za hujuma ambazo
hupangwa kila unapofika wakati wa uchaguzi ambapo watu hushambuliwa, kutekwa na kufanyiwa
vitendo vibaya.
Post a Comment