ad

ad

Msanii afungiwa, Giggy na Sanchi kujisalimisha

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, imemfungia kujihusisha na kazi za sanaa, msanii Pretty Kind kutokana na uvunjifu wa maadili.

Taarifa hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Michezo Juliana Shonza alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, na kueleza kwamba msanii huyo haruhusiwi kufanya kazi za muziki au sanaa yoyote kwa kipindi cha miezi sita, iwe ya jukwaani au kutoa kazi mpya.

Adhabu hiyo imefuatia baada ya msanii huyo kupiga picha za utupu na kuzipost instagram, kitendo kilichoonekana ni uvunjifu wa maadili ya Mtanzania, ambacho kimeanza kupingwa vikali na serikali ya awamu yatano.

Sambamba na msanii huyo, serikali pia imewataka msanii Giggy Money na mwanamitindo Sanchoka maarufu kama Sanchi, kujisalimisha kutokana na kosa la kupiga picha za utupu na kuziweka kwenye mitandao ya kijamii.

Hivi karibuni Rais Magufuli alizitaka mamlaka husika kuwachukulia hatua wasanii wanaokiuka maadili, kwa kuvaa mavazi ya nusu utupu na kupiga picha za nusu utupu.

No comments

Powered by Blogger.