ad

ad

Maskini Wastara! Apewa Makavu na Msanii Cloud 112, Kisa Pesa!

BAADA ya waraka wa staa wa filamu, Wastara Juma kuanikwa mitandaoni ukionesha kudhulumiwa na watu mbalimbali ikiwemo ishu ya yeye kwenda Sweden kucheza filamu, staa wa filamu, Issa Mussa ‘Cloud’ ameibua jipya sakata hilo. 


Akizungumza, Cloud alisema kwamba ameshtushwa na waraka huo ambao mashabiki wameuchukulia tofauti kwa kumuona ni tapeli na alimuita Wastara Sweden kumfanyisha filamu bila malipo.

 “Niliongea naye vizuri kuwa aje Sweden nitamgharamia malazi, usafiri na kila kitu na kwamba tukimaliza kutengeneza filamu na ikaingia sokoni ndiyo tutakuja kulipana,” alisema Cloud. 


Wastara alidaiwa kuandika waraka huo ulioonesha kusaidiwa matibabu ambapo ndani yake alidai kutapeliwa Sh. Mil 80 na kampuni ya simu, waandaaji wa filamu na pia kwenda kufanya filamu Sweden na kurudi mikono mitupu.

No comments

Powered by Blogger.