ad

ad

MAHAKAMA YAAMURU SUGU Na MASONGA WAENDE RUMANDE MPAKA

Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Joseph Mbilinyi 'Jongwe' pamoja na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga wakiwa kwenye gari la polisi.Kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Joseph Mbilinyi 'Jongwe'  pamoja na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga imetajwa leo Jumanne tarehe 16 Januari, 2018 katika Mahakama ya Mkoa wa Mbeya na mahakama imewanyima dhamana na kuamuru wapelekwe rumande mpaka tarehe 19 Januari 2018.
Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga akisalimia wanahabari (hawapo pichani).Baada ya kesi hiyo kutajwa na watuhumiwa kukana shitaka, hakimu aliamuru dhamana iko wazi kwa watuhumiwa ndipo wakili wa serikali akaiambia mahakama iwaweke ndani watuhumiwa kwa ajili ya usalama wao na walikuwa wakifuatiliwa na kuna viashiria vya usalama wao kuwa mdogo na pia sababu nyingine iliyotolewa ni kwamba Mbunge Mbilinyi alikiuka masharti kwa kutoripoti jana kwenye Ofisi za polisi Mkoa ambapo ushahidi wa barua ya kuomba ruhusa na kuruhusiwa na RPC ukatolewa lakini ubishani ukapelekea Hakimu kuamuru atatoa uamuzi wa dhamana hiyo tarehe 19 Januari 2018 kutokana na wafanyakazi wa mahakama waliopaswa kuandika rulling wako wilayani kikazi hivyo tarehe 19 Januari ndipo mahakama itatoa uamuzi.
Kesi hiyo ambayo watuhumiwa wanasimamiwa na Wakili msomi Boniface Mwabukusi ilifunguliwa kutokana na maneno waliyotoa katika hotuba zao walizotoa katika Mkutano wa Hadhara wa Mbunge huyo wa Mbeya Mjini uliofanyika tarehe 30 Disemba, 2017 katika kiwanja cha Shule ya msingi Mwenge iliyopo katika Kata ya Ruanda jijini Mbeya.
Awali baada ya Mkutano huo waliitwa na Jeshi la Polisi mkoani Mbeya tarehe 02 Januari 2018 na kuhojiwa pamoja na kuchukuliwa maelezo na baada ya hapo waliripoti mara kadhaa na leo ndio imetajwa mahakamani kwa mara ya kwanza.
Habari - CHADEMA
Kanda ya Nyasa

16 Januari, 2018
ALUTA CONTINUA.



No comments

Powered by Blogger.