Kheri James: Rais Magufuli Ameamua Kusafisha Nyumba Hakuna Mende Atakayebaki
Na Mathias Canal, Arusha
Umoja
wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa umesifu utendaji wa
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kutokana na
uwajibikaji wake katika kuimarisha chama pamoja na serikali kwa maslahi
ya watanzania.
Kauli
hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Umoja huo ambaye pia ni Mjumbe wa
Kamati kuu ya CCM Taifa Ndg Kheri Denice James wakati akizungumza na
wakazi wa Kijiji cha Mndarara kilichopo Kata ya Ngaranaibor akiwa
ziarani Wilayani Longido Mkoa wa Arusha kwa ajili ya kampeni za Ubunge
katika Jimbo la Longido.
Kheri
alisema kuwa Rais Magufuli na Mwenyekiti wa CCM Taifa ameamua kusafisha
nyumba ambayo ni nchi ya Tanzania hivyo hakutegemewi mtu yeyote kusalia
kama mende wa kumkwamisha katika umaridadi wa usafi huo wa maslahi ya
Taifa.
Mjumbe
huyo wa kamati kuu ya CCM Taifa aliwasihi wananchi kujitokeza kwa wingi
tarehe 13 Januari 2018 kupiga kura kwa wingi zitakazompa ushindi
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Longido kupitia Chama Cha Mapinduzi Dkt
Steven Kiruswa ili kutekeleza ilani ya ushindi wa chama hicho ya Mwaka
2015-2020 ambayo ni mkataba muhimu kati ya wananchi na CCM.
Alisema
kuwa serikali inapaswa kuchukua hatua Kali za kisheria dhidi ya yeyote
atakayetaka kuvuruga ama kuleta uvunjifu wa amani Siku ya uchaguzi.
"Ndugu
zangu wana Mrandarara nataka niwasihi na kuwahakikishia kuwa MTU yeyote
atakayeleta masihara na mchezo mchezo Siku ya uchaguzi anapaswa
kuchezewa yeye mchezo mpaka ashike adabu" Alikaririwa Kheri
Alisema
kuwa Mara baada ya Mbunge kuchaguliwa tu anapaswa kusimamia vyema
asilimia 5% za fedha za mfuko wa vijana zinazotolewa na Halmashauri
sambamba na asilimia 5% kwa ajili ya wanawake ili kuendeleza chachu na
imani ya vijana na wananchi kwa ujumla dhidi ya serikali yao.
Aliongeza
kuwa kumchagua mbunge wa CCM itampendeza zaidi Rais na Mwenyekiti wa
CCM Taifa Mhe Magufuli kwani atakuwa amepata msaidizi kwa ngazi ya Jimbo
atakayetekeleza vyema ilani ya CCM ambayo imeainisha mambo mengi muhimu
na msingi kwa maslahi ya watanzania wote hasa wananchi wa Longido.
Uchaguzi
wa Ubunge Jimbo la Longido na majimbo mengine matatu likiwemo Jimbo la
Singida Kaskazini na Songea Mjini utafanyika tarehe 13 Januari 2018.
Wakati
huo huo akiwa Kijijini Mairowa Kata ya Ngarenaibor Mwenyekiti Kheri
amewataka mawakala wa CCM kote nchini kuwa waaminifu katika kusimamia
vyema chaguzi mbalimbali kote nchini kwani wameaminiwa na Chama hivyo
kutojihusisha na viashiria vya aina yoyote ya rushwa.
Post a Comment