Katibu Mkuu CHADEMA Awajibu Wanaodai Ameshindwa Kuimudu Nafasi Hiyo
Katibu
Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Vincent Mashinji
amesema kuwa yeye yuko tofauti na makatibu wengine wa vyama.
Ameyasema
hayo Jijini Dar es salaam wakati akifanya mahojiano na kituo kimoja cha
Televisheni, ambapo amesema kila kiongozi huwa na mikakati yake ya
kiutendaji.
Amesema kuwa wapo baadhi ya watu wanaosema amepooza, mkimya, hana mikiki mikiki kama walivyo viongozi wengine.
“Ukichanganya
majukumu yangu ya kikazi na yale aliyokuwa akifanya Dkt. Slaa unaweza
kuharibu mipango ya kitaasisi,” amesema Dkt. Mashinji.
Hata
hivyo, amezitaja baadhi ya kazi alizozifanya akiwa Katibu Mkuu kuwa ni
pamoja na uandaaji wa Katiba ya Chadema pamoja na miongozo mbalimbali.
Post a Comment