Breaking News: Babu Seya, Papii Watinga Ikulu, Dar, kumshukuru Rais Magufuli
Rais John Magufuli (katikati) akiwa ameshikana mikono akiomba dua na mwanamuziki Nguza Vicking “Babu Seya” (wa pili kushoto) na wanaye Johnson Nguza “Papii Kocha” (wa pili kulia), Francis Nguza (wa kwanza kulia) na Michael Nguza (kushoto) walipofika Ikulu Dar leo, Januari 2, kumshukuru kwa msamaha aliotoa kwao dhidi ya kifungo cha maisha walichokuwa wakitumikia.
“Babu Seya” na wanaye Johnson Nguza “Papii Kocha”, Francis Nguza na Michael Nguza walipofika Ikulu leo.
Rais Magufuli alitoa msamaha kwa wanamuziki hao, miongoni mwa watu zaidi ya 8,000 aliowasamahe siku ya uhuru wa Tanzania Bara, Desemba 9 mwaka jana, wakati akilihutubia taifa huko Dodoma.
Post a Comment