Babu Tale Amfunda Shilole na Mumewe
Meneja
wa WCB na Tip Top Connection, Babu Tale ambaye alikuwa msimamizi wa
ndoa kati ya Shilole na Uchebe, amewataka pindi wanapopishana katika
ndoa yao kutopeleka mambo hayo katika mitandao ya kijamii.
Tale amesema endapo watafanya hivyo wasifike kwake ila kama ugomvi utakuwa wa ndani kwa ndani wasisite kufika wake.
“Kama
unampenda usigombane naye kwenye mitandao, kwa hiyo kama mnagombana na
mpenzi wako mnaenda kugombania Instagram, mtaachana na kwangu usije,”
Tale amemueleza Uchebe.
“Kama mkigombania chumbani njoo kwangu any time tutayamaliza, kama mnagombania kwenye mitandao hayo si mapenzi,” amesisitiza.
Hata
hivyo amesema si kwamba anamkataza kujidai na mkewe katika mitandao ila
anapaswa kutambua kuwa amezungukwa na mbwa mwitu ambao kazi yao ni
kuharibu maendeleo ya ndoa za watu.
Post a Comment