UVCCM: Huu si wakati wa kuabudu cheo cha Mtu
Akizungumza
na wanachama wa CCM na jumuiya zake visiwani Zanzibar, alisema huu ni
wakati wa kufanya kazi kwa ushirikiano badala ya kumuabudu mtu kutokana
na cheo chake.
Alisema
kiongozi anayejitambua ni yule anayefanya kazi kwa maslahi ya vijana
wenzake na kilichobaki kwa sasa ni kupambana ili jumuiya hiyo ya vijana
iweze kufika mbali kwa maslahi ya vijana na taifa kwa ujumla.
Aidha,
alisema wakati wa vijana wanaopenda kulalamika umefika mwisho hivyo ni
vyema wakajitahidi kufanya kazi bila ya upendeleo na woga.
Aliwataka
viongozi wenzake katika jumuiya hiyo kuanza kuhakiki mali za chama na
aliyekuwa haendani na kasi ya chama hicho awapishe wanaoweza.
"Umegombania nafasi na tumekupa, sasa tufanyeni kazi ili vijana wajue thamani ya uongozi," alisema.
Kheir
alisema uhakiki wa mali za chama hicho kwa upande wa Zanzibar utafanywa
na Wazanzibari wenyewe na atahakikisha anapatiwa ripoti ya uhakika
kwenye taarifa watakazozipeleka kwa uongozi wa juu na uhakiki wa
watumishi hewa pia utaangaliwa.
Makamo
Mwenyekiti wa Umoja huo, Tabia Maulid Mwita, alisema yupo tayari
kufanya kazi kwa ushirikiano wa hali ya juu na vijana wote na
kuwashukuru kwa kumchagua kushika nafasi hiyo na kuendeleza ahadi zake
alizoziahidi kipindi cha kampeni.
Aidha,
aliwataka vijana kuacha makundi kwa kuwa uchaguzi umekwisha hivyo
atahakikisha haki inatendeka bila ya kumuonea mtu wala kujali cheo chake
na kufanya maamuzi kwa matakwa yake bila ya kumshauri mtu.
"Vijana
ndio jeuri ya chama ila kwa anayejitambua na sio kukaa kutukana katika
majukwaa kijana mzuri ni yule anayependa kusikiliza ushauri wa wakubwa
wake," alisema.
Mapema
akitoa utambulisho kwa viongozi, Kaimu Katibu wa Umoja huo Zanzibar,
Abdulghafar Idirissa Juma, alisema Umoja huo utaangalia upya vitega
uchumi vyake ili viweze kuleta tija kwa wanachama na kuiendeleza jumuiya
yao.
Akizungumzia
mradi wa Darajani alisema kuwa ulihodhiwa na baadhi ya viongozi wa
serikali hivyo alimtaka Mwenyekiti wa Umoja huo kulifuatilia suala hilo
ili mipango iendelee na mradi huo uweze kuleta tija kwa vijana na taifa
kwa ujumla.
Post a Comment