Nuh Mziwanda Noma Aijibu Ndoa Ya Shilole
Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’.
Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichopo karibu na wawili hao kilivujisha picha hizo na kueleza kuwa, wawili hao kwa sasa wapo kwenye dimbwi zito la mahaba, kwani mwanadada huyo kafa kaoza kwa baba Anya ambaye ni mzazi mwenziye na Nawal waliyemwagana baada ya ndoa yao ya Kiislamu kuvunjika.
Suzan Michael ‘Pretty Kind’.
“Si unajua Shilole kaolewa? Jambo hilo limechangia pia Nuh kuamua kuuweka moyo wake kwa Pretty ili asiumie sana kwani ni mwanamke ambaye alimpenda sana” aliongeza Baada ya kuzinyaka picha hizo zinazowaonyesha wawili hao wakiwa wamepozi kimahaba paparazi wetu alianza kumvutia waya Nuh ambaye simu yake iliita bila kupokelewa, kwa upande wake Pretty Kind alipotafutwa alistaajabu shushushu wetu kuzinasa picha hizo na kuomba apigiwe baadaye.
Baada ya muda alipotafutwa alikuwa na haya ya kusema; “Nuh ni mpenzi wangu ndiyo, sioni tatizo katika hilo, nampenda na yeye naamini ananipenda, kwa kipindi kirefu nimekuwa nikimmezea mate hatimaye sasa amekuwa wangu.”



Post a Comment