Ndugu Wa Babu Seya Wamiminika Gerezani, Wamshukuru Jpm
BAADA ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli kutoa msamaha kwa familia ya Nguza Viking aliyekuwa amehukumiwa
na mwanaye Papii Kocha kifungo cha maisha, ndugu wa familia hiyo na
marafiki wamefurika nje ya Gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam na
kumshukuru Rais.
Mtandao huu umenasa baadhi ya picha zinazoonesha tukio zima eneo hilo hadi kuachiwa wanamuziki hao maarufu ambao tayari wameingia uraiani.
“Tunamshukuru Mungu, tunamshukuru sana Rais Magufuli kwa kuwasamehe ndugu zetu. Mungu ambariki,” alisema Mbangu, mtoto wa Babu Seya.
Babu Seya na Papii wameachiwa leo baada ya kutumikia kifungo hicho kwa takriban miaka 13 katika Sherehe za Miaka 56 ya Uhuru zilizofanyika mkoani Dodoma hii leo.

Post a Comment