ad

ad

Mzungu Kumbadili Dini Sasha, Wadaiwa Kufunga Ndoa Hivi Karibuni.

Sasha Kassim
MUUZA nyago machachari Bongo, Sasha Kassim ambaye anatarajia kufunga pingu za maisha siku chache zijazo, inasemekana kuwa yupo mbioni kubadili dini kumfata Mzungu wake aitwaye Boniface, kutoka kwenye dini yake ya Kiislamu na kuwa Mkristo.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, mwanadada huyo japo anaipenda dini yake, amelazimishwa kumfuata Mzungu huyo vinginevyo ndoa itaota mbawa.

Alipotafutwa Sasha alikataa kuhusu kumfuata Mzungu huyo; “Tumevutana sana lakini kwa kweli mimi ni ngumu, atanifuata yeye tu naamini.”

No comments

Powered by Blogger.