ad

ad

Lema Ahudhuria Mazishi ya Mbwa wa Nassari


Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (aliyeshikilia mbwa kushoto) akishiriki na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (kulia) kumwombea mbwa huyo kabla ya kumzika kwenye kaburi lake lililo mbele.  Mbwa huyo alipigwa risasi na watu wasiojulikana baada ya kuvamia nyumba ya Nassari usiku kuamkia jana.
Mbwa huyo aliyekufa baada kupigwa risasi.
Mwonekano wa karibu wa jeraha baada ya risasi kumwingia mbwa huyo.

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema mapema leo asubuhi na Mbunge wa Arumeru Mashariki,  Joshua Nassari, na waombolezaji wengine wachache wamehudhuria mazishi ya mbwa wa Nassari aliyeuawa na watu wasiojulikana baada ya kuvamiwa nyumbani kwake na kumpiga risasi.

Mazishi hayo yamefanyika huko huko Arumeru.Mbwa huyo alikuwa ni mlinzi wa Nassari nyumbani kwake ambapo amesikitishwa na kifo cha mnyama huyo aliyekuwa rafiki wake wa karibu.

No comments

Powered by Blogger.