ad

ad

Britney Spears Ajiachia na Serengeti Boy Wake 'Waromatika Live"

INGAWA ni mwanzoni tu mwa Desemba, tayari in­aonyesha staa wa Pop, Britney Spears, amesha­ianza sikukuu, juzikati alituma picha kwenye mitandao ya ki­jamii akionekana yupo ‘kloz’ na mpenzi wake, anayemzidi kwa umri wa miaka 12.


Staa huyo wa Pop alipata w a t o t o hao na mume wake wa zamani, Kevin Federline, ambaye alikuwa naye tangu 2004 hadi 2007. Spears pia aliwahi kutoka na bwanamdogo Justin Timberlake kwenye miaka ya 2000.

 Britney, 35, alionekana akiwa katika mapozi mbalimbali ya kimahaba na mpenzi wake huyo, Sam Asghari, 23, kabla ya kuanza kucheza na kuonyesha j in si walivyoupamba mjengo wao uli­opo jijini California, kwa mapam­bo ya Krismasi.

Britney, ni mama wa watoto wawili, licha ya kumzidi Sam miaka 12, penzi lao linaonekana imara. Mapema wiki iliyopita, wawili hao walionekana wakiwa na watoto wa Brit, Sean, 12 na Jayden James, 11, uwanjani wakishuhudia mch­ezo wa kikapu kati ya LA Lakers na Golden State Warriors.



No comments

Powered by Blogger.