Wema Afanya Vituko Mahakamani
Miss Tanzania 2006 na msanii wa filamu za Kibongo, Wema Sepetu jana alitinga mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar kwa ajili ya kusikiliza kesi inamkabili ya matumizi ya madawa ya kulevya ambapo mrembo huyo baada ya kufika kwenye viunga vya mahakama hiyo alipokelewa na mapaparazi waliokuwa wakimpiga picha.
Wema baada ya kuwaona mapaparazi hao alianza kuwatembelea kwa pozi huku akiwalaumu kuwa walikuwa wakimkera ambapo baada ya kuona wanazidi kumuandana alisimama kwenye mlango wa gari dogo alimokuwa mama yake na kuwawekea pozi wamfotoe wakimaliza waondoke.
Vituko vya Wema havikuishia hapo alipotoka kwenye gari alimuokuwa mama yake alimchukua na kwenda nae kwenye ukumbi wa kusikiliza kesi yake huku wakiwa wameshikana mikono.
Wakiwa kwenye ukumbi wa mahakama hiyo mapaparazi waliendelea kumpiga picha ambapo nae aliwageuzia kibao na kuanza kuwarekodi na simu yake ambapo mapaparazi hao walianza kuogopa walivyokuwa wakirekodiwa.
Hata hivyo kesi hiyo haikuweza kuendelea ambapo iliahirishwa mpaka Novemba 24 mwaka huu itakapotajwa tena mahakamani hapo.
Post a Comment