Serikali Yasema Haiwezi Kuajiri Vijana Wote Nchini
Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Peter Mavunde.
Mh. Mavunde ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Aida Joseph Kenani lililohoji,
serikali ya awamu ya tano imepunguza wafanyakazi kwenye kada mbalimbali kwa kigezo cha kutokuwa na sifa. Je, ni lini sasa serikali itatoa ajira kwa kuwapa kipaumbele vijana wa nchi ambao kwa sasa ni wengi wamerundikana mtaani.
“Katika azma ya kutengeneza nafasi nyingi za ajira hasa kwa kundi kubwa hilo la vijana serikali, imekuja na mipango mikakati mbalimbali, si kweli kwamba tunaweza tukawa tuna nafasi za kuwaajiri wote kwenye sekta ya umma, ndiyo maana kupitia programu nilizozisema serikali imeona ni vyema kuishirikisha sekta binafsi, lakini na kuona falsafa ya uchumi wetu wa viwanda lakini vilevile kuwahamasisha vijana kushiriki katika sekta za uzalishaji mali ikiwemo kilimo ufugaji na biashara, ili kwa pamoja tuwe tumetengeneza nafasi nyingi kwa vijana ili tuwafanye vijana wengi wa Kitanzania kuamini kwamba nafasi za kazi ni lazima ziwe za maofisini,” amesema Mavunde.
“Kwa mujibu wa sera ya ajira, sera ya ajira imezungumza vyema kabisa tafsiri ya neno ajira maana yake ni shughuli yoyote halali inayompatia mtu kipato, kwa hiyo serikali tunachokifanya ni kutengeneza nafasi nyingine zaidi za ajira ili vijana wengi zaidi wapate nafasi za kujiajiri na kuwaajiri vijana wengine.”

Post a Comment