Samia Suluhu Amtembelea Tundu Lissu Nairobi Hospital
Samia Suluhu akimjulia hali Lissu.
Samia amtembelea Lissu baada ya kumalizika kwa hafla ya kumwapisha Rais Uhuru Kenyatta kuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya katika uwanja wa Moi Kasarani Mjini Nairobi.
Mhe. Samia Suluhu Hassan alimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Lissu alikimbizwa katika hospitali hiyo baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 na watu wasiojulikana nyumbani kwake, Area D, Mjini Dodoma, Septemba 7 mwaka huu.
Post a Comment