Ruge Afungukia Ndoa Ya Zamaradi Mketema
Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.
Hatimaye Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba amezungumzia suala la ndoa ya mama watoto wake, Zamaradi Mketema kumpa mateso kutokana na ndoa yake.
Ruge alifunguka kuhusu suala hilo jana, ikiwa ni wiki kadhaa tangu isambae sauti iliyoaminika kuwa ni ya kwake, akisikika akizungumza na Zamaradi kwenye simu huku akilia kwa sauti ya mateso akilalama kuachwa.
Akizungumza katika kipindi cha 360 cha Clouds TV jana asubuhi, Ruge alisema mwanaume muungwana, hazungumzii masuala ya ndani ya mahusiano yake ya kimapenzi, akitumia msemo wa kiingereza kuwa ‘Gentlemen don’t kiss and tell’.
Zamaradi Mketema akiwa na mume wake Shabani.[/caption]Ruge alisema alikuwa anafahamu kila kilichokuwa kinaendelea kuhusu ndoa ya Zamaradi na kwamba alimpa baraka zote, tofauti na ilivyokuwa ikizungumzwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa ameshtukizwa na kuumizwa. “Kila kilichofanyika nilikuwa na taarifa na kilikuwa na baraka zangu.
Ni sehemu ya maisha tunapitia. Kubwa kuliko yote, nina watoto wawili ambao nimezaa na Zamaradi. Ninamheshimu mno na hadi sasa naendelea kumheshimu mno,” Ruge alisema.
“Unajua kama kuna kitu nitakufundisha (mtangazaji) kama mdogo wangu , ‘When you are a gentleman, you don’t kiss and tell’ (Ukiwa mwanaume muungwana, haubusi na kusimulia).
Vitu vingine vinabaki kuwa vyako binafsi vya ndani,” aliongeza. Ruge ameeleza kuwa hata wikendi iliyopita alikuwa na watoto wake aliozaa na Zamaradi na kwamba anawapenda sana na hataacha kumheshimu mama yao. Alisema alilazimika kulizungumzia hilo ili kuweka kumbukumbu sawa kufuatia maneno yanayoendelea kuzungumzwa mitandaoni. Zamaradi aliolewa wiki kadhaa zilizopita na kuzua mjadala mzito, tukio ambalo lilionekana kuwa la ghafla na lisilotarajiwa, hasa baada ya kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na Ruge kwa muda mrefu.
NA MWANDISHI WETU | RISASI MCHANGANYIKO

Post a Comment