Mwigulu ashangaa upinzani kuweka wagombea
Waziri wa Mambo ya Ndani na Mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi CCM Mwigulu Nchemba amewashangaa vyama vya upinzani kwa kuweka wagombea katika uchaguzi mdogo wa madiwani nchini kwani kwasasa ilani inayofanya kazi ni ya CCM na kwamba
Waziri Mwigulu alipokuwa kwenye Kampeni Siuyu - Singida Mashariki
hao wagombea wao wataenda kutekeleza ilani gani.
Hayo ameyasema akiwa katika kata ya Siuyu jimbo la Singida Mashariki wilaya ya Ikungi alipokuwa akifungua kampeni za mgombea Udiwani kupitia tiketi ya CCM baada ya diwani Gerald Mahami aliyekuwepo wa CHADEMA kuvuliwa uongozi kutokana na kutoshiriki vikao vya baraza la madiwani la halmashauri ya Ikungi
Waziri Mwigulu amesema uchaguzi wa mwaka 2015 kila mtu alileta mgombea wake akiamini atashinda na baadae mgombea wa CCM Rais Dr Johm Magufuli alishinda na ilani ya CCM ndiyo inayotekelezwa hivyo haoni haja ya wapinzani kusimamisha mgombea kwani kwasasa ilani hiyo ya CCM ndiyo inayofanya.
Waziri Mwigulu amesema kwamba watu kuwa na vyama vingine si kosa na wala kuwa na kadi ya chama kingine si lazima upigie chama chako bali upige kura kwa diwani ambaye ilani yake ndio inatekelezwa kwa wakati huo ambapo atakuletea maendeleo.
"Tulipokuwa kwenye uchaguzi Mkuu kila chama kilikua na sera zake na kila mtu alikuwa na wagombea wake huku kila chama kikiamini kwamba kitashinda ngazi zote.
Sasa kwenye uchaguzi huu mdogo hatunadi ilani kwani inayotumika ni hii ya CCM.
Wenzetu wangekuwa wanatambua wale waliotufundisha siasa za vyama vingi wanafanya nini.
Tutakuwa wa ajabu kama unajua huu ni msikiti halafu unampeleka Mwinjilist akafanye nini na atatekeleza ilani gani? Siyo vibaya kuwa upinzani lakini unapaswa kutazama ni ilani gani inayotekelezwa kwa sasa" Mh. Nchemba
CHANZO: EATV

Post a Comment