ad

ad

Muna: Nitafunga Mpaka Lulu Atoke

MMOJA kati ya wasanii wa karibu wa staa wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ni Rose Alphonce ‘Muna’ ambaye tangu aanze kukumbana na tatizo hili la kesi ya mauaji bila ya kukusudia dhidi ya msanii mwenzake marehemu Steven Kanumba amekuwa naye bega kwa bega.

Muna ni miongoni mwa wasanii wa filamu zao la Kaole ambaye amejitolea kuwa kama dada wa hiari kwa Lulu, ameonyesha moyo wa kipekee kuliko msanii yeyote Bongo ambapo amekuwa karibu kuanzia siku ya kwanza ya kesi ya Lulu mpaka siku ya hukumu.

Ijumaa limemtafuta Muna na kuzungumza naye mengi juu ya ukaribu huo ambapo amesema kuwa amepokea hukumu ya Lulu ya miaka miwili jela kwa masikitiko makubwa sana lakini kitu anachoamini hilo ni jaribu tu itafika wakati litapita na ataendelea na maisha yake mengine.

“Unajua mimi namuamini sana Mungu,naamini kabisa hilo ni jaribu na ipo siku litapita na Lulu ataendelea na maisha yake ya zamani kama kawaida,” anasema Muna.

Muna anaongeza kuwa, atakumbuka sana kipindi chote alichokuwa na Lulu, katika mambo mbalimbali waliokuwa wakifanya pamoja kwenye shida na kwenye raha ambapo walipita naye pamoja lakini kubwa atakalolifanya ni kufunga na kumuombea usiku na mchana. “Nitakumbuka nyakati zote nilizokuwa naye pindi yupo uraiani. Kuanzia siku aliopewa huku kazi yangu moja tu sasa kufunga na kuomba kwa ajili yake,” anasema Muna.

No comments

Powered by Blogger.