Dk Shika Amzimikia Ray C Kwa Kuimba na Kucheza

Rehema Chalamila ‘Ray C’.
DAKTARI Louis Shika ambaye alipata umaarufu mkubwa baada ya jaribio lake la kununua nyumba za mfanyabiashara Said Lugumi, ametoa mpya baada ya kudai kuwa anaguswa na muziki wa mkongwe Rehema Chalamila ‘Ray C’.

“Ukiniuliza ni msanii gani wa muziki wa Kitanzania ambaye namkubali, sipati kigugumizi kukuambia kwamba ni Ray C, kwake sijiwezi, napenda anavyoimba, anavyocheza na kadhalika, wimbo ninaoupenda zaidi ni ule uitwao ‘Nataka Niwe Nawe Milele’ wa msanii huyo,” alisema Ray C
Post a Comment