Sanga ampa shavu Mayay Bodi ya Ligi
MWENYEKITI wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Clement Sanga amemteua nahodha wa zamani wa Yanga, Ally Mayay kuwa mjumbe wa Kamati mpya ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Ofisa Mtendaji Mkuu, Boniface Wambura, Sanga ameteua kamati hiyo ya TPLB inayoshughulikia uendeshaji na usimamizi wa ligi mbalimbali.
Ligi hizo ni Ligi Kuu Bara, Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL). Kamati hiyo itaongozwa na Sanga mwenyewe akiwa mwenyekiti, huku Makamu Mwenyekiti akiwa ni Shani
Mligo, Katibu ni Wambura na wajumbe ni Mayay, Issa Batenga, Leslie Liunda na Wakili Saleh Njaa.
Wajumbe wengine ni George Malawa, Dk Ellyson Maeja, Isaac Chanji, Baruan Muhuza na Mbakileki Mutahaba. Wakati huohuo, Sanga amewateua wajumbe wawili kuingia kwenye Kamati ya Uongozi ya TPLB.
Wajumbe hao ni Kanali Charles Mbuge ambaye ni Mwenyekiti wa Ruvu Shooting na Abuu Changawa ‘Majeki’.
Kwa mujibu wa Ibara ya 28 (vi) ya Kanuni za Uendeshaji) za TPLB, mwenyekiti ana nafasi ya kuteua wajumbe wawili kuingia kwenye Kamati ya Uongozi.
Hivi karibuni, Sanga ambaye ni Kaimu Mwenyekiti wa Yanga alichaguliwa kwa kishindo nafasi ya uenyekiti wa TPLB akimshinda Yahya Mohammed wa Mtibwa Sugar.

Post a Comment