Mshindi Wa Nyumba Atikisa Dar, Mapokezi Yake Si Ya Kitoto
Wafanyakazi wa Global Groups Ltd wakijiandaa kumpokea Mshindi wa Nyumba, George Majaba aliyewasili Dar es Salaam kutoka Dodoma.
Majaba akiwasili kwenye ofisi za Global.
Majaba akisalimiana na Mkurugenzi wa Makampuni ya Global Groups Ltd, Eric Shigongo, kushoto ni Meneja Mkuu, Abdallah Mrisho.
Wafanyakazi wa Global wakiwalaki majaba na mkewe baada ya kuwasili ofisini hapo.
“Niwe mkweli, kama zawadi hii angeipata mtu ambaye tayari ana nyumba tano, nisingefurahi kabisa, lakini kwa mujibu wa makala zako nilizokuwa nasoma, wewe unaishi kwenye nyumba ya kupanga, kwa maana hiyo siku zote ulikuwa ukiomba upate nyumba na leo Mungu amekubariki.
“Wewe utakuwa balozi mzuri wa Global Group kwa sababu watu wengi wamekuwa wakisema kuna ujanjaujanja katika zawadi, nina uhakika kabla ya leo hakukuwa na mtu yeyote unayemjua hapa, lakini wewe umejikuta ukipata nyumba. Tunakukaribisha sana na asante Mungu kwa ndoto zetu kutimia,” alisema.
Baada ya kukaribishwa na kuzungumza machache na wafanyakazi na baadaye kutembezwa katika vitengo mbalimbali vya Global Group, Majaba na familia yake waliondoka kuelekea Bunju B, ambako ndipo ilipo nyumba yake ya kisasa na hivyo kuwa miongoni mwa wamiliki halali wa nyumba za kisasa katika Jiji la Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu.
















Post a Comment