Mateso Ya Hamisa Mobeto baada ya Kuelekezwa Na Diamond
SIKU chache baada ya mwanamitindo Hamisa Mobeto kumburuza mahakamani mzazi mwenzake kudai fi dia ya malezi ya mtoto, Ijumaa Wikienda limebaini mateso yanayompata mrembo huyo ambayo ndiyo yaliyomsukuma kufungua kesi hiyo kusaka ahueni ya maisha. Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili ulibaini kuwa, Hamisa anapambana kusaka matumizi mengi yanayomfanya ashindwe kuhimili suala la malezi. Katika udadisi wake, Ijumaa Wikienda lilimfi kia mmoja wa marafi ki wa karibu wa Hamisa aliyeomba hifadhi ya jina ambapo alisema kinachompa mateso mrebo huyo ni gharama za kununua ‘pampers’, maziwa, mavazi na mafuta.
“Wewe vuta picha, maziwa peke yake tu yanauzwa shilingi elfu ishirini kwa kopo moja. Hayo maziwa hayamalizi wiki yameisha, sasa hebu piga ishirini mara mwezi, mara miezi sita je?S asa hapo ndipo penye shughuli. Piga elfu hamsini mara nne kwa wiki nne
ANATUMIA YA BEI
“Tena sasa si unajua Hamisa alishazoea kuishi kistaa, hataki kunyonyesha. Alibadili na kuanza kumpa mtoto maziwa ambayo ni ya bei mbaya, yanauzwa elfu hamsini ambayo yanafanana kabisa na ya mama.
tayari laki mbili hiyo, mara miezi sita je? Unafi kiri hiyo pesa inatoka wapi?” Alisema shosti huyo wa Hamisa. Kama hiyo haitoshi, kitu kingine ambacho kimekuwa ‘kaa la moto’ kwa Hamisa tangu mzazi mwenzake asitishe huduma baada ya kujifungua, rafi ki huyo alisema ni pampers. “Hiyo ndiyo usiseme. Pampers ni gharama asikwambie mtu. Yaani si chini ya elfu hamsini anatumia kwa ajili ya pampers kila wiki. Ukipiga kwa mwezi nayo inakwenda kwenye laki mbili hivi.
MAVAZI
“Yaani kwa kweli ninyi msione hivi, mavazi yanamtesa Hamisa, yule mtoto anataka kumlea kistaa kutokana na jina lake (Hamisa). “Analazimika kununua nguo Mlimani City na kwenye maduka makubwamakubwa ya nguo za watoto, inacheza kwenye shilingi elfu 60 mpaka laki, sasa Hamisa atazitoa wapi? Hapo ndipo mawazo yanapomtesa, akaamua kuliamsha dude la mahakamani,” kilisema chanzo.
GHARAMA ZA HOSPITALI
Chanzo hicho kilizidi kunyoosha maelezo kwa kusema mbali na chakula na malazi, kingine kilichompa mawazo ni gharama za hospitali hususan katika kipindi hiki cha uchanga. “Ni lazima uwaze sana hadi kichwa kipasuke kwa maisha haya ya sasa ukifi kiria mtoto anahitaji maziwa, anahitaji kuvaa, anahitaji mafuta, sabuni zake, kichwa lazima kipasuke kwa mawazo,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kuelemewa na mzigo huo, Hamisa kupitia kwa mawakili wake, Abdullah Lyana na Walter Godluck wa Kampuni ya Uwakili ya Century Attorneys, aliamua kumuandikia mzazi mwenzake huyo wito wa kufi ka Mahakama ya Watoto Oktoba 30, mwaka huu. Katika suala hilo, Hamisa alidai alipwe shilingi milioni 5 kila mwezi au zaidi kulingana na mahakama itakavyoamua. Kama hiyo haitoshi, Hamisa alitaka alipwe shilingi milioni 30 kama gharama za mtoto hadi sasa.
Post a Comment