ad

ad

Mastaa Nigeria waliotekwa na penzi la mameneja wao



WAFUATAO ni wanamuziki wanaofanya vizuri Nigeria waliojikuta wakitekwa na kuzama penzini na mameneja wao Nigeria na kutawala kwenye vichwa mbalimbali vya habari za burudani.

 Kwenye listi hiyo yumo mwanamuziki wa Injili, Lara George ambaye alikuwa anatoka na meneja wake Gbenga George ambapo baadaye ndiye alimuoa.


 Yupo pia Tiwa Savage na meneja wake Tunji Balogun ‘Teen Beez’. Wawili hawa walianza kutoka kimapenzi kabla ya kuoana. Wengine ni mwanamuziki J’odie na meneja wake David Nnaji ambao kwa sasa pia wameoana na wana mtoto mmoja, huku mwanamuziki Yemi Alade na meneja wake Taiye Aliyu wakiwa hawako nyuma maana penzi lao kwa sasa linatajwa kushika kasi! 

Kwenye listi hii yumo pia Wizkid na meneja wake Jada P, huku mwanamuziki Banky W ingawa anatarajia kumuoa Adesua Etomi lakini anasemekana kuwa kwenye penzi zito pia la mwanadada, Eniola Akinbo ‘Niyola’ ambaye anamsimamia kwenye kazi zake za muziki

No comments

Powered by Blogger.