ad

ad

Makosa 3 Mabaya Wanayoyafanya Wanawake Kwa Wanaume

MAPENZI ni maelewano. Mapenzi ni kusikilizana. Vinapokosekana hivyo vitu viwili muhimu, penzi linakosa uhai. Litakuwa linayumba kama gari lisilokuwa na dereva. Nini kitatokea kama gari litakuwa linakwenda bila dereva? Litaanguka! Uhusiano mzuri ni ule ambao, mwanamke anamsikiliza mwanaume na mwanaume hivyo hivyo anamsikiliza mwanamke pale inabobidi. Kila mmoja amheshimu mwenzake. Ampe thamani na hadhi ya kibinadamu. Wengi wetu huwa tunakosea, tunajipendelea. Tunakuwa wabinafsi. 

Tunajipa thamani wenyewe na kuwasahau wenzetu. Hilo ni kosa kubwa. Ni vyema zaidi ukampa thamani mwenzako, huo ndiyo upendo. Tena si upendo tu wa kibanadamu, Mungu pia ametutaka tuifanye hivyo. Mjali na umthamini mwenzako kama au zaidi ya unavyojijali na kujithamini mwenyewe.

Ukiyafanya hayo, hakika hata kama unaowatendea hivyo hawatakutendea na wewe lakini kwa mapenzi ya Mungu utapata baraka zake. Utaona mambo yanavyokunyookea, niamini mimi! Nirudi katika kiini cha mada yangu. Kuna mambo ambayo wanaume wanayakosea kwa wanaume na kusababisha uhusiano upoteze uelekeo lakini kwa leo, nitakupa makosa matano ambayo wanawake wanayakosea kwa wanaume. Kwa wewe msichana ambaye unahitaji au upo tayari kwenye uhusiano ni vyema sana ukayafahamu makosa haya, itakusaidia ukiyajua maana pengine unayafanya kwa kutokujua au kwa bahati mbaya.

KUZUNGUMZA SANA
Wanaume wengi hawapendi mwanamke muongeaji au mapepe sana. Hata kama wewe ni fundi wa kupiga soga na mashosti zako, ukiwa kwa mumeo unashauriwa kuzungumza kwa staha. Weka kituo baada ya kuzungumza maneno mawili, matatu. Siyo mwanamke unaongea weee, hupumziki? Mwanaume anataka kusikia maneno machache na yenye kutia moyo, kufariji. Maneno yanayotamkwa kwa lugha ya kubembeleza, kuchombeza kiasi cha kumtoa
mawazo yote aliyokuwa nayo kichwani. Kwa uhalisia wanaume wana majukumu mazito ya utafutaji japo natambua wapo pia wanawake wana majukumu mazito tu. Wanaume wanavurugwa kwelikweli, wanachokitarajia siyo makelele mengi bali maneno yanayoshuka kwa mpangilio mzuri. Usiwe mropokaji sana.

 KUMZINGUA FARAGHA
Hili nalo ni kosa. Wanawake wengi huwa wana kasumba ya utayari wa faragha. Mwanaume anakuwa na uhitaji, mwanamke anasema amechoka. Bahati mbaya sana, wengine husema wamechoka wakati tayari wapo dimbani na wameshaanza kupashapasha mwili. Tendo la ndoa lina umuhimu wake, usiwe mtu wa kutoa udhuru mara kwa mara. Jitahidi umpe haki yake pindi inapohitajika. Wewe ndiyo mtu wake, ukiwa mvivu wa kumpa unafikiri atapewa na nani? Nini kitatokea kama kila wakati utakuwa mtu wa kutoa udhuru? Atachepuka kama si mvumilivu.

KUTOMPA HESHIMA MWANAUME
Wanaume wengi huwa wanapenda kuheshimiwa. Nisisitize,
kuheshimiwa na si kuogopwa. Mwanaume ambaye kwa nadharia ya Kiafrika inaaminika kwamba ndiyo kichwa, ukimheshimu atakupenda zaidi. Anapenda utambue ‘ukichwa’ wake katika familia. Mara kadhaa nimekuwa nikiandika, kuna madhara gani mwanamke akimheshimu mwanaume wake? Jibu unalo, mheshimu mume wako bila ya kuweka kisingizio chochote. Ukimheshimu inavyostahili, nakuhakikishia, atakupenda daima.

Heshima ni kitu kidogo sana lakini kina maana kubwa sana katika uhusiano. Mheshimu mwanaume wako, hata kama unaona amekukosea, tumia hekima na lugha ya rafiki kuzungumza naye. Ukitumia busara na kumuonesha mwanaume kwamba unameshimu, hakika atakusikiliza hata kama alikuwa amekasirika kiasi gani. Kwa leo inatosha, siku nyingine nitazungumzia makosa ya wanaume kwa wanawake. Waweza nifuata kwenye ukurasa wangu wa Instagram na Twitter kwa jina la Erick Evarist.

No comments

Powered by Blogger.