Kesi ya Lulu Yaunguruma, Mdogo wa Kanumba Asimulia Ugomvi Siku ya Tukio (Video)
Elizabeth Michael ‘Lulu’. |
KESI inayomkabili mwigizaji maarufu wa Bongo Muvi, Elizabeth Michael
‘Lulu’ kuhusishwa na kifo cha aliyekuwa staa wa filamu nchini, Steven
Kanumba imeanza kuunguruma tena leo Alhamisi, Oktoba 19 katika Mahakama Kuu
Kanda ya Dar es Salaam.
Katika kesi hiyo inayosikilizwa mbele ya Jaji Sam Rumanyika, ushahidi
upande wa Jamhuri ulitolewa na mdogo wa marehemu Kanumba, Seth Bosco,
ambaye alikuwa shahidi wa kwanza.
Akijibu
swali la wakili wa utetezi, Peter Kibatala, shahidi Seth ameieleza mahakama
hiyo juu ya ugomvi alioushuhudia kati ya Elizabeth Michael na marehemu Steven
Kanumba siku ya tukio.
Seth
ameieleza mahakama kwamba anachofahamu yeye ni kuwa palikuwa na mgogoro
kati ya Lulu na Kanumba aliousikia, uliosababishwa na simu kwamba, Lulu alikuwa
akiongea kwa simu na mwanaume mwingine hali iliyozua ugomvi huo.
Mbali na
Seth, shahidi wa pili aliku,,wa ni daktari ambaye hata hivyo hakufika
mahakamani hapo kwa kuwa aliomba udhuru kwa madai kuwa anaumwa. Jaji Rumanyika
ameiahirisha kesi hiyo hadi kesho saa tatu. Mashahidi waliobaki ambao ni watatu
watatoa ushahidi wao.
Baadhi ya watu waliofika kusikiliza kesi hiyo ni mama mzazi wa Lulu, Lucresia
Karugila, mama mzazi wa Kanumba, Flora Mtegoa, muigizaji Dkt. Cheni na
wengine.
Lulu anakabiliwa na kesi ya kusababisha kifo cha Kanumba bila kukusudia,
mnamo Aprili 7, 2012 .
Post a Comment